STARS IPO KAMILI KUKIPIGA NA CRANES

STARS IPO KAMILI KUKIPIGA NA CRANES

Like
255
0
Friday, 03 July 2015
Slider

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeondoka nchini mwao kuelekea Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya jumamosi.

Kikosi cha Taifa Stars kimeaondoka kikiwa na wachezaji 20,na viongozi 7 wa bechi la ufundi,Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wamefanya mazoezi vizuri katika kipindi chote cha maandalizi, na sasa wako tayari kwa mchezo huo, mipango ikiwa ni kupata ushindi siku ya jumamosi.

Wachezaji Abdi Banda na Mohamed Hussein wameacha katika msafara huo kwa sababu ya kuwa majeruhi

Comments are closed.