STEVEN GERRARD: DAVID BECKHAM NI SHUJAA WANGU

STEVEN GERRARD: DAVID BECKHAM NI SHUJAA WANGU

Like
253
0
Wednesday, 08 July 2015
Slider

Steven Gerrard amesema kuwa aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake katika kikosi cha England David Beckham amehusika kwa kiasi kikubwa kwenye uhamisho wake kwenda kuichezea LA Galaxy.

Beckham amekaa Los Angeles na kushinda kombe la MLS katika mchezo wa mwisho uliochezwa December 2012.

Gerrard, 34, anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wamexico siku ya jumamosi.

“David ni shujaa wangu, ni mtu hodari sana, mchezaji mzuri, ni mtu niliemtegemea kujifunza na kupata ushauri wake kabla sijafanya maamuzi ya kujiunga na LA Galaxy”

Gerrard ambae alikataa dili ya mwaka mmoja mapema mwaka jana na baadae kutangaza kuiaga klabu yake iliyomlea ya Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita ambapo hivi sasa amethibitisha kwenda kuitumikia Galax.

 

 

Gerrard atavaa jezi yake namba nane kama kawaida ambapo atakutana na Robbie Keane mchezaji aliyewahi kukipiga nae Liverpool ambae alijiunga na timu hiyo tangu mwaka 2011.

 

Gerrard ameonyesha kuwa mwenye furaha kujiunga na Keane ambae tayari amemtambulisha kwa wachezaji wengine kikosini hapo.

Comments are closed.