SUDANI KUSINI: NUSU YA WATOTO WAKATISHA MASOMO

SUDANI KUSINI: NUSU YA WATOTO WAKATISHA MASOMO

Like
226
0
Wednesday, 13 January 2016
Global News

 

SHIRIKA linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto walioko Sudan kusini hawako shule.

 

Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani.

 

Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani na kwamba tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane zimeteketea.

Comments are closed.