SYLAS MWAKIBINGA AJIONDOA BODI YA LIGI KUU

SYLAS MWAKIBINGA AJIONDOA BODI YA LIGI KUU

Like
423
0
Tuesday, 04 November 2014
Slider

Mtendaji wa bodi ya  TFF inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza, Sylas Mwakibinga ameamua kuachana na kibarua chake kwenye taasisi hiyo nyeti ya soka nchini.

Uchunguzi wa E.sports umegundua kwamba Mwakibinga ameamua kuachia ngazi katika nafasi yake kutokana na mvutano mkubwa unaoendelea kati ya rais wa TFF -Jamali Malinzi na wakali Damas ndumbaro aliyezawadiwa kifungo cha miaka 7 kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje nchi kwa madai ya kutoa siri nzito zilizojificha ndani ya shirikisho wakati akivitetea vilabu kupinga agizo la makato ya asilimia tano ya fedha ya mdhamini.

E.sport imefanya mahojiano na wajumbe wa bodi hiyo ya ligi, Charz Mguto, uthibitisho juu ya hatua ya Mwakibinga kujiengua kwenye wadhifa wake.

hata hivyo E.spot ikamtafuta silas Mwakibinga mwenyewe kutaka kujua kilichojificha nyuma ya pazia kuhusu kuondoka kwake

Comments are closed.