Tony Hage ameishi Liberia kwa zaidi ya miaka hamsini. Na ndipo mahali alipo kutana na mke wake kisha kuanzisha biashara yake yenye mafanikio. Aliendelea kuishi Liberia katika kipindi ambacho raia wengi wa nchi hiyo wali kimbia ili kuepuka machafuko akilenga kuiona nchi anayoipenda ikipata mafanikio. Mpaka sasa bwana Hage si raia wa Liberia, amezuiwa kupata uraia wa kudumu wa nchi hiyo kwa sababu ya rangi ya ngozi yake na asili ya familia yake kutoka huko Lebanon. ‘Tutakuwa watumwa’ Nchi ya...
Wakili na mwanaharakati mzaliwa wa Kenya ambaye alilazimishwa kwenda uhamishoni nchini Canada mwezi Februari mwaka huu alitarajiwa kurejea mjini Nairobi siku ya Jumatatu Machi 26, 2018 huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda asiruhusiwe na serikali ya Kenya kuingia nchini. Katika taarifa aliyoituma kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika siku ya Jumapili akiwa mjini London Uingereza, Miguna Miguna alisema kuwa ataingia Kenya hata bila pasipoti au viza kumruhusu kufanya hivyo. “Ndege yetu itatua Nairobi Jumatatu saa nane na dakika...
Watu 37 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi. Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41. Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka. Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry. Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema. Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka...
Binti mmoja wa Kipalestina aliyekamatwa baada ya kumchapa kofi mwanajeshi, Msichana huyo Ahed Tamimi alikiri kuwa na hatia kwa makosa manne aliyokuwa akishtakiwa kati ya 12 yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo shambulio la mwili, wakili wake ameeleza. Kadhalika, atalipa faini ya shekeli 5,000 sawa na dola 1,440 . Binti huyo mwenye miaka 17 alikamatwa baada ya kunaswa kwenye picha ya video akiwakabili wanajeshi wawili nje ya nyumba yake mwezi Desemba. Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa ataachiwa huru kipindi cha majira ya joto...