Imekuwa kawaida kwa bingwa wa Kombe la Dunia kutolewa hatua ya makundi, lakini hakuna aliyetegemea hilo lingetokea kwa Ujerumani. Ujerumani haikuwahi kutolewa katika hatua ya makundi katika miaka 80 iliyopita. Korea Kusini wameilaza kwa mabao 2-0 na kuitupa nje katika Kombe la Dunia katika hatua ya makundi. Maana yake wameivua ubingwa. Kipigo hicho kimezua hofu kubwa kwa mashabiki wa timu hiyo ya taifa na huo ndiyo ukweli usiopingika. 1998: France alikuwa bingwa 2002: France alitoka hatua ya makundi 2006:...
Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimesafisha makosa yake iliyoyaonyesha katika mchezo wa kwanza dhidi ya Switzerland kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Costa Rica leo. Mabao ya Brazil yamewekwa kimiani katika dakika za nyongeza kuelekea mchezo kumalizika kupitia kwa Philippe Countinho na Neymar Jr. Ushindi huo umemfanya Neymar ashindwe kuamini matokeo hayo baada ya kumwaga machozi ya furaha baada ya kufunga bao la pili. Katika kundi E Brazil imeongoza kwa kuwa na alama 4 ikifuatiwa...
Michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inaendelea tena Jumapili ya leo kwa jumla ya mechi tatu kupigwa. Brazil ambao wametwaa ubingwa wa mashindano hayo mara tano watakuwa wanacheza na Switzerland, wakati Ujerumani watakuwa wanakipiga na Mexico. Ratiba kamili ya mechi za leo hii hapa....
Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia. Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 12 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu. Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43′ minutes, 90’+1), Dzyuba (71′ ) na Golovin (90’+4)....
Kombe la dunia linaanza siku tisa zijazo kuanzia leo. Afrika inawakilishwa 5 katika mashindano hayo yanayochezwa nchini Urusi na wachambuzi wanasema Afrika inayo nafasi zamu hii. Leo tunakuletea makundi ya timu hizi Kundi A Kundi hili lina mwenyeji wa mashindano nchi ya Urusi na Saudi Arabia, Misri na Uruguay. Ndani ya kundi hili Urusi ndio nchi pekee iliyo chini kisoka katika viwango vya FIFA ikishika nafasi ya 65 wakifuata Saudi Arabia, nafasi ya 63, Misri na Uruguay wakiongoza kundi hili...