MASHABIKI wa soka walijipanga katika mtaa mashuhuri jijini Paris uitwao Champs-Elysees jana na kuipokea kifalme timu ya soka ya nchi hiyo iliyobeba Kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kuishinda timu ya Croatia. Mapokezi hayo yaliyokuwa ya kifalme yalipambwa na kina aina ya shamra akiwemo rais Emmanuel Macron na mkewe. Miongoni mwa taswira kubwa zaidi ilikuwa ni rangi za taifa hilo ambazo zilionekana kutawala macho ya kila mtu — nyeupe, bluu na nyekundu. Paul Pogba akiwa na Kombe la Dunia...