TAIFA STARS VS MALAWI

TAIFA STARS VS MALAWI

Like
333
0
Monday, 30 March 2015
Slider

Katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana kwenye uwanja wa Ccm Kirumba Mwanza kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya taifa ya Malawi (The Flames) na kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1 wadau wamekuwa na maoni tofauti kufuatia matokeo hayo.

Malawi ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango Stars katika dakika ya tatu ya mchezo kupitia mchezaji wake Esau Kanyenda goli lililodumu hadi kipindi cha pili cha mchezo.

Matumaini ya watanzania waliokuwa wakifatilia mchezo huo yaliletwa na mshambuliaji wa Tp Mazembe ya Drc Mbwana Samatta aliposawazisha bao hilo la Malawi katika dakika ya 79 ikiwa ni pasi nzuri iliyotengenezwa na Mrisho Ngasa alieingia kipindi cha pili akitokea benchi akichukua nafasi ya Haroun Chanongo

Harakati za stars kutafuta bao la ushindi wakiwa nyumbani hazikuzaa matunda richa ya kuliandama lango la The Flames mara kadhaa katika dakika za mwisho za mchezo huo hivyo basi mchezo kumalizika kwa sare ya moja kwa moja.

Comments are closed.