TAMISEMI YAZITAKA TAARIFA ZA VURUGU KATIKA CHAGUZI ZA SELIKARI ZA MITAA ZIWASILISHWE

TAMISEMI YAZITAKA TAARIFA ZA VURUGU KATIKA CHAGUZI ZA SELIKARI ZA MITAA ZIWASILISHWE

Like
413
0
Monday, 15 December 2014
Local News

WAZIRI WA NCHI Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI- Mheshimiwa HAWA GHASIA ameitaka mikoa ambayo vurugu zimejitokeza wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa kuwasilisha taarifa za matukio hayo ili maamuzi sahihi yafanyike kwa wahusika ikiwemo kuwafukuza kazi.

Mheshimiwa GHASIA ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa za awali kuhusu uchaguzi huo katika ngazi ya mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika jana disemba 14 mwaka huu nchini.

Aidha katika taarifa hiyo ameitaja baadhi ya mikoa iliyopata dosari kupitia zoezi la uchaguzi kuwa ni pamoja na Kilimanjaro, Manyara, Morogoro na mkoa wa Shinyanga.

 

Comments are closed.