TANESCO IMETAKIWA KULITUMIA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA

TANESCO IMETAKIWA KULITUMIA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA

Like
468
0
Monday, 14 December 2015
Local News

SHIRIKA la Umeme Nchini (Tanesco) limetakiwa kuandaa mpango madhubuti wa utitirishaji maji kutoka kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu ili kuwepo na maji ya kutosha kuzalisha umeme kwenye vituo vya Hale na New Pangani.

 

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa agizo hilo wakati  wa ziara yake katika mabwawa ya kuzalishia umeme ya Hale na Pangani yaliyoko mkoani  Tanga na bwawa la Nyumba ya Mungu la mkoani Kilimanjaro.

 

Agizo hilo alilitoa baada ya kujionea namna ambavyo kina cha maji kwenye mabwawa hayo kimepungua kutokana na mipango hafifu ya utiririshaji maji

Comments are closed.