TANESCO NA REA WATOLEA UFAFANUZI UCHELEWESHWAJI WA MRADI WA UMEME MKURANGA

TANESCO NA REA WATOLEA UFAFANUZI UCHELEWESHWAJI WA MRADI WA UMEME MKURANGA

Like
544
0
Monday, 24 November 2014
Local News

SHIRIKA la umeme nchini -TANESCO kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini –REA wametoa ufafanuzi juu ya kuchelewa kwa ukamilikaji wa Mradi wa Umeme katika vijiji vya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

Akizungumza na EFM Ofisini kwake jijini Dar es salaam Meneja wa-TANESCO Kanda ya Dar es salaam na Pwani MAHANDE MUGAYA amesema tatizo hilo linatokana na ufinyu wa Bajeti iliyowekwa kwa kuwa haikidhi mahitaji ya Umeme unaohitajika.

Amewatoa hofu wananchi wa Vijiji hivyo kwa kuwa mradi huo unatarajia kukamilika mapema mwezi Januari mwakani kama walivyopanga kufuatia Serikali kuwaongeza kiasi cha fedha kwa ajili ya Mradi huo.

 

Comments are closed.