TANESCO YAWAWEKA WAZEE KIZANI

TANESCO YAWAWEKA WAZEE KIZANI

Like
306
0
Wednesday, 19 November 2014
Local News

KITUO cha Kulea Wazee wasiojiweza cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya Morogoro kinakabiliwa na tatizo la Umeme kwa takribani miezi miwili sasa na kuwafanya kuishi kwa shida bila kujua muafaka wao kutoka Serikalini.

Akizungumza na EFM Mwenyekiti wa Wazee hao JOSEPH KANIKI ameeleza kuwa wamekuwa wakikatiwa Umeme mara kwa mara na Shirika la Umeme Tanzania –TANESCO kwa kutolipa bili kwa muda mrefu huku wakiamini Shirika hilo na Serikali wana mawasiliano mazuri.

KANIKI amebainisha kuwa kukosekana kwa umeme kunawafanya kushindwa kujihudumia hasa nyakati za usiku kutokana na Wazee wengine hawawezi kutembea na wanapokuwa kwenye giza wanashindwa kwenda haja ndogo na hata kubwa.

 

Comments are closed.