Tanzania imeandika historia mpya baada ya kukamilisha mchakato wa kutengeneza Rasimu pendekezwa ya Katiba Mpya na kuikabidhi kwa Rais JAKAYA KIKWETE pamoja na Rais wa Zanzibar Dokta ALLI MUHAMMED SHEIN.
Akitoa hotuba yake kwa Maelfu ya Wananchi,Mabalozi waliowakilisha nchi zao pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na Kidini, Rais KIKWETE anaeleza
Mbali na hayo amewasihi wajumbe waliofanya kazi ya kutunga na kurekebisha katiba kutambua na kuwa mabalozi wazuri katika kupigania na kutimiza wajibu wa kuwaelimisha wananchi juu ya katiba hiyo
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dokta ALLI MOHAMED SHEIN amesema kuwa ni jambo la kujivunia kuwa na Katiba inayojali Makundi yote katika jamii