TANZANIA NA NAMIBIA KUSIMAMIA USALAMA AFRIKA

TANZANIA NA NAMIBIA KUSIMAMIA USALAMA AFRIKA

Like
197
0
Monday, 12 October 2015
Local News

RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Namibia Dokta Hage Gottfried Geingob, wameahidi kuwa watasimamia kwa juhudi nchi za bara la Africa ili kuhakikisha zinakuwa na usalama wa kisiasa na  kiuchumi hata watakapo maliza muda wao wa uongozi ili wananchi wake waweze kuishi kwa amani.

Akizungumza Ikulu Jijini Dar es Salaam  wakati akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Dokta Kikwete amesema kuwa  endapo viongozi  wakubwa wa Africa wakiweza kuwakomboa wananchi wao kutoka kwenye umaskini, njaa na magonjwa bara hilo litakuwa limejikomboa na kuwa na usalama wa kisiasa na hata kiuchumi.

Comments are closed.