TANZANIA YAAHIDI KUCHUKUA HATUA 5 ZA KUTETEA NA KUENDELEZA HAKI ZA WANAWAKE

TANZANIA YAAHIDI KUCHUKUA HATUA 5 ZA KUTETEA NA KUENDELEZA HAKI ZA WANAWAKE

Like
232
0
Monday, 28 September 2015
Local News

TANZANIA imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, kwa kufuta sheria kandamizi kwa wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia.

 

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kufuta na kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni vinavyoendeleza ubaguzi kwa wanawake ikiwemo Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.

 

Msimamo huo umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, nchini Marekani.

Comments are closed.