TANZANIA YAWA NCHI YA KWANZA KWENYE MIONGONI MWA NCHI WANACHAMA WA SADC NA EAC KUINGIA KWENYE MFUMO WA DIJITI

TANZANIA YAWA NCHI YA KWANZA KWENYE MIONGONI MWA NCHI WANACHAMA WA SADC NA EAC KUINGIA KWENYE MFUMO WA DIJITI

Like
237
0
Friday, 03 April 2015
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania-TCRA,imesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC pamoja na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC katika kutumia mfumo wa matangazo wa Dijiti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Meneja Mawasiliano wa TCRA-INNOCENT MUNGI,amesema nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano ya Simu Duniani-ITU,kwa pamoja zimeridhia makubaliano ya kusimamisha mfumo wa Utangazaji wa television unaotumia Teknolojia ya Analojia katika Miundombinu ya minara Junin 17 mwaka huu.

Amebainisha kuwa kutokana na makubaliano hato nchi mbalimbali zimeamua kuchukua hatua za pamoja kuhakikisha zinahama kutoka katika mfumo wa Analojia kwenda Dijiti.

Comments are closed.