Tanzia: Profesa wa Upasuaji Chuo Kikuu Muhimbili Afariki Dunia

Tanzia: Profesa wa Upasuaji Chuo Kikuu Muhimbili Afariki Dunia

Like
1015
0
Monday, 18 June 2018
Local News

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof. Adrea Pembe anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Leonard Lema kilichotokea leo asubuhi tarehe 18 Juni 2018 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Prof. Lema alikuwa ni Profesa katika Idara ya Upasuaji katika Skuli ya Tiba MUHAS. Wakati wa uhai wake, Prof. Lema ametumikia Chuo katika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Mkuu wa Idara ya Upasuaji mwaka 2003 mpaka 2006. Profesa Lema pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kati ya mwaka 2006 na 2010.

 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach kwa ushirikiano kati ya familia na MUHAS na ratiba kamili itatolewa mara tu itakapokamilika.

Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na jumuia ya MUHAS wanaungana na familia ya marehemu Prof. Lema katika kuomboleza msiba huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na:
Ofisi ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano, MUHAS
18 Juni, 2018.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *