Mamlaka nchini Indonesia imesema kuwa ifikapo Ijumaa ya Oktoba 5 itasitisha utafutwaji wa manusura wa tetemeko na tsumani iliyotokea mwishoni mwa juma lililopita katika kisiwa cha Sulawesi.
Takriban watu 1400 wamefariki, lakini maofisa wanasema idadi inatarajiwa kuongezeka zaidi.
Rais wa Indonesia Joko Widodo ametembelea kwa mara ya pili kisiwa hicho na kusema juhudi za utafutwaji wa manusura zinaridhisha.
Misaada inaingia katika maeneo yaliyoathirika kupitia uwanja wa ndege wa Palu licha ya kuwa nao uliharibika kwa kiasi.
Baadhi ya wahanga wa tukio hilo sasa wanaweza kupata maji safi na chakula.