TFF YAFANYA YAFANYA MAREKEBISHO YA MECHI LIGI DARAJA LA KWANZA

TFF YAFANYA YAFANYA MAREKEBISHO YA MECHI LIGI DARAJA LA KWANZA

Like
689
0
Thursday, 16 October 2014
Slider

UWANJA+WA+ALI+HASSAN+MWINYI

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, imefanya marekebisho ya mechi nne za kundi A za Ligi Daraja la kwanza ili kutoa fursa ya matumizi ya uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.

Timu za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Octoba 25 kwenye uwanja wa mabatini mkoani Pwani sasa zitacheza Octoba 26 uwanja wa Karume, Dar es salaam.

Nayo mechi ya Polisi Dar es salaam na majimaji ya Songea ilikuwa ichezwe Octoba 26 sasa itachezwa Octoba 27, huku mechi ya Friends rangers na Ashanti UNITED ilikuwa ichezwe mabatini mkoani pwani, Octoba 26, sasa itachezwa uwanja wa Karume octoba 28

mechi nyingine ni kati ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Octoba 25 kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele na itachezwa octoba 26 kwenye uwanja huohuo

 

Katika hatua nyingine TFF imeongeza muda wa usajili wa wachezaji kwa timu za ligi daraja la pili kwa sikun saba, ambapo sasa utamalizika octoba 21 mwaka huu

Awali usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike octoba 14 mwaka huu lakini ni klabu chache zilizoweza kusajili ndani ya muda uliopangwa.

Klabu ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakiwa kukamilisha ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili

Comments are closed.