TFF YAONGEZA MPUNGA KWA BINGWA WA KOMBE LA FA

TFF YAONGEZA MPUNGA KWA BINGWA WA KOMBE LA FA

Like
537
0
Thursday, 31 May 2018
Sports

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeongeza zawadi ya mshindi wa Kombe la Shirikisho ‘Azam Sports Federation Cup’ ili kuzidi kuongeza hamasa ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho hilo, Clifford Ndimbo, amesema kuwa zawadi ya mshindi wa Kombe hilo atatwaa kiasi cha shilingi milioni 50 huku wa pili akichukumia milioni 10.

Aidha, Ndimbo ameeleza kutakuwa na zawadi nyingine zitatoka katika vipengele mbalimbali ikiwemo ya mchezaji bora, mfungaji bora pamoja na mlinda mlango bora wa michuano hiyo.

Ni siku moja pekee kesho Ijumaa iliyosalia kuelekea fainali ya mchezo huo utaowakutanisha Singida United dhidi ya mtibwa Sugar FC utakaopigwa Juni 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Tayari timu zote zimeshawasili jijini humo huku wadau wengi wa soka wakiusubiria mtanange huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni huku Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *