Timu ya Watoto wa Kike Waishio Mazingira Magumu Watoa Kipigo Kikali kwa Wamarekani

Timu ya Watoto wa Kike Waishio Mazingira Magumu Watoa Kipigo Kikali kwa Wamarekani

Like
740
0
Monday, 14 May 2018
Sports

 

Timu ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kutoka Tanzania, imewatandika timu ya watoto kama hao kutoka Marekani, kwa mabao 5-0 katika mashindano ya Street Children World Cup na kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Street Child United, timu ya watoto wa kike wa Tanzania imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya nusu fainali, ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja naikiwa haijafungwa goli hata moja, na kuweka rekodi ya kipekee.

Mchezo wa timu ya Tanzania dhidi ya Marekani, umefanyika katika Uwanja wa Timu kubwa ya Soka ya Lokomotive Moscow jijini Moscow nchini Urusi ambapo mshambuliaji wa Tanzania, Yasinta Peter anaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi, ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao 5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *