SERIKALI ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo imeeleza kuwa taarifa zilizopo kwa sasa zinaashiria kwamba makundi ya kigaidi ikiwemo Islamic State, Al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.
Hata hivyo, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa wa mashambulio hayo.