TPC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA POSTGIRO

TPC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA POSTGIRO

Like
442
0
Tuesday, 18 November 2014
Local News

SHIRIKA la Posta TPC wamebadilishana makubaliano ya msingi waliyoyaingia na kampuni ya simu ya Zantel ya huduma mpya ya biashara iitwayo POSTGIRO leo jijini Dar es salaam.

Huduma hiyo mpya ya kibiashara ya kukusanya na kulipa fedha kwa niaba ya kampuni, shirika, kiwanda au taasisi za serikali na binafsi itarahisisha ulipaji wa ada, amana, gawio, kodi, pensheni, michango na mishahara.

Akizungumza na waandishi wa habari jiijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa TPC DEOS MNDEME amesema inaridhisha kutambua kuwa TPC na Zantel wanamadhumuni yanayofanana ya kutumia teknolojia mpya za mawasiliano ya pamoja.

Nae Mkurugenzi wa Shughuli za Kibiashara wa Zantel MOHAMED MUSSA amefafanua namna wananchi watakavyofaidika na huduma hiyo iliyomlenga mwananchi wa chini.

Kwa upande wake Meneja mkazi wa TPC Zanzibar MWANAISHA ALI amebainisha kuwa ubia huo utasaidia kurahisisha huduma za posta kama inavyofanya huduma ya Esypesa kwa sasa.

 

Comments are closed.