TRA NA POLISI WAKAMATA MAKONTENA 9

TRA NA POLISI WAKAMATA MAKONTENA 9

Like
319
0
Tuesday, 01 December 2015
Local News

MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA-kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata Makontena tisa ambayo bado haijafahamika yana vitu gani ndani katika eneo la Tangibovu Mbezi Beach Jijini Dar es salaam yaliyosafirishwa kinyume na utaratibu usiku wa manane.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa Mlipa kodi kutoka-TRA-Richard Kayombo amesema Mamlaka imebaini kuwa Muagizaji wa makontena hayo ni Heritage Empire Company Limited na wakala wa Forodha aliekuwa akishughulikia ni Napock Africa Company Limited ambao hawajaweza kupatikana mara moja.

Kufuatia hali hiyo TRA wametoa saa 24 kwa mmiliki kujitokeza ili mzigo uweze kufunguliwa kabla ya kuamua kuyataifisha kwa mujibu wa sheria.

Comments are closed.