TRA YANASA SHEHENA KUBWA YA BIDHAA ZA MAGENDO

TRA YANASA SHEHENA KUBWA YA BIDHAA ZA MAGENDO

Like
307
0
Friday, 12 February 2016
Local News

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali ya Ukanda  wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na mipakani.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo katika mahojiano maalum yaliyofanyika  ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.

 

Amesema kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi milioni kumi kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za forodha .

Comments are closed.