TRA YANASA CD NA DVD ZA MUZIKI NA FILAMU ZISIZOLIPIWA KODI

TRA YANASA CD NA DVD ZA MUZIKI NA FILAMU ZISIZOLIPIWA KODI

Like
333
0
Tuesday, 01 March 2016
Local News

MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA-kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imefanya ukaguzi wa stempu za kodi kwenye kazi za wasanii na kufanikiwa kukamata CD na DVD za Muziki na filamu 7, 780 ambazo hazina stempu za kodi.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake.

Kayombo amesema kuwa msako huo ulioanza Februari 26 katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam umebaini ukiukwaji wa sharia kutoka kwa wasambazaji wa kazi za wasanii wa nyimbo na filamu.

Comments are closed.