TRUMP ABADILI MSIMAMO WAKE JUU YA KUTOA MIMBA

TRUMP ABADILI MSIMAMO WAKE JUU YA KUTOA MIMBA

Like
286
0
Thursday, 31 March 2016
Global News

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda mfupi baada ya kusema wanawake wanaotoa mimba wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba ukiharamishwa.

 

Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC kauli ambayo ilimfanya kushutumiwa vikali.

 

Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa. Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu 1973 .

Comments are closed.