Trump kumchagua balozi mpya wa UN mwezi huu

Trump kumchagua balozi mpya wa UN mwezi huu

Like
504
0
Wednesday, 10 October 2018
Global News

Rais Donald Trump wa Marekani amesema atafanya maamuzi katika kipindi cha wiki mbili ama mapema zaidi kuhusu kumchagua balozi mpya akayeiwakilisha Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema atafanya maamuzi katika kipindi cha wiki mbili ama mapema zaidi kuhusu kumchagua balozi mpya akakayeiwakilisha Marekani katika Umoja wa Mataifa. Balozi wa sasa Nikki Haley ametangaza kujiuzulu wadhifa huo jana, na rais Trump amekubaliana na uamuzi huo.

Nikki Haley, balozi wa sasa wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa alitangaza kuachia ngazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Aligusia kwenye barua yake ya kujiuzulu kwamba anatarajia kwenda kwenye sekta binafsi baada ya miaka miwili akihudumu kama balozi wa Umoja wa Mataifa, na kabla ya hapo miaka sita ya kuwa gavana wa South Carolina.

Miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuteuliwa na rais Trump ni mshauri msaidizi wa zamani wa masuala ya usalama wa taifa Dina Powell na aliyewahi kuwa afisa wa ngazi za juu wa serikali ya rais George Bush Goldman Sachs, ambaye ni mshirika wa karibu wa binti wa rais Trump, Ivanka Trump na mkwe wake, Jared Kushner.

Alipokutana na waandishi wa habari katika ikulu ya White House kutangaza rasmi uamuzi wa Haley, rais Trump akasema “Sawa. Dina ni mtu ambaye ninamfikiria pia. Tuna majina mengi, na unajua, Nikki alikuwa na uwezo mkubwa. Nikki ataendelea kufanya kazi na sisi na kutusaidia kumchagua mrithi wake. Pia, atatusaidia kwenye uchaguzi wa 2020. Nikki ni rafiki yangu mkubwa. Amefanya kazi nzuri kwa hivyo atahusishwa.

Taarifa za kujiuzulu kwa Haley zimewashangaza baadhi ya washirika muhimu wa Marekani na wabunge wengi wa Republican wanaohusika na masuala ya sera za kigeni. Lakini pia imekuja ikiwa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya chaguzi za katikati ya muhula.

Baadhi ya mabalozi wa Umoja wa Mataifa pia wameshtushwa na kusikitishwa na maamuzi ya Haley waliyefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa, hata wakati walipotofautiana. Vassily Nebenzia ni balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, “Ninasikitika anaondoka kwa sababu tulifanya kazi nzuri na tulikuwa na mashirikiano ya kibinafsi, licha ya tofauti tulizokuwa nazo. Lakini kwa kuwa bado yupo, na lilikuwa ni tangazo tu la kujiuzulu, bado tutakuwa na muda mzuri wa kuwa pamoja kabla ya kuhitimisha muda wa kuwa balozi wa Marekani hapa.

Trump alisema amesikia jina la Ivanka likitajwa kama mmoja ya wanaotarajiwa kuziba pengo hilo. Ingawa alimsifia binti yake kuwa mwenye uwezo mkubwa, lakini alisema iwapo atamchagua angeshutumiwa kwa upendeleo. Balozi ya Marekani nchini hapa Richard Grennell pia anatajwa.

rais Trump na Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa wakiwa ikulu ya White House

Haley aliteuliwa kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa mwezi Novemba 2016.

Akiwa balozi alifanikiwa kuongoza juhudi za serikali yake za kukabiliana na kile walichodai kuwa hatua za umoja huo zinazopingana na Marekani na Israel, ambazo ni pamoja na uamuzi wa Marekani kuondoka kwenye baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa na kusimamisha ufadhili kwenye shirika la kuhudumia wakimbizi wa Palestina, UNRWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *