UCHAGUZI MKUU: VYOMBO VYA HABARI VYAPONGEZWA

UCHAGUZI MKUU: VYOMBO VYA HABARI VYAPONGEZWA

Like
246
0
Tuesday, 10 November 2015
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa taarifa kwa wananchi hasa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza na viongozi wa menejimenti ya wizara na taasisi zake kwenye kikao cha kazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Profesa Gabriel amesema kuwa kipindi cha uchaguzi vyombo vya habari vimefaya kazi kubwa ya kuwapa habari za uchaguzi wananchi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao na hivyo kuwawezesha wananchi kujua mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea.

Comments are closed.