UCHAGUZI UGANDA: MUSEVENI AONGOZA MATOKEO YA AWALI

UCHAGUZI UGANDA: MUSEVENI AONGOZA MATOKEO YA AWALI

Like
343
0
Friday, 19 February 2016
Local News

MATOKEO ya awali yaliyotangazwa  hii leo nchini Uganda yanaonyesha rais wa muda mrefu  wa nchi hiyo amempita mpizani wake mkuu katika uchaguzi wa rais nchini humo.

 

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya Uganda, rais Yoweri Kaguta Museveni amejipatia takriban asilimia 62 ya kura, akimpita mpinzani wake mkubwa Kizza Besigye aliyejipatia asili mia 33 ya kura.

 

Matokeo hayo yanahusu asili mia 23 ya vituo vyote vya kupiga kura nchini humo ambapo Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa kesho jumamosi.

Comments are closed.