UFARANSA: AKATAZWA KUVAA HIJABU KAZINI

UFARANSA: AKATAZWA KUVAA HIJABU KAZINI

Like
290
0
Thursday, 26 November 2015
Global News

MAHAKAMA ya Ulaya ya haki za binaadamu imekataa hoja ya mfanyakazi mmoja wa kiislamu aliyetaka kuvaa hijab kazini.

Christine Ebrahimian alipoteza kazi yake katika hospitali moja ya Paris baada ya kusisitiza kutaka kuvaa hijab huku hospitali hiyo ikisema kuwa imepokea malalamiko kuhusu yeye kutoka kwa wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo.

Sheria ya Ufaransa inakataza maonyesho ya uhusiano wowote wa kidini na wafanyakazi wa umma ambapo pia mahakama hiyo imesema kuwa haiwezi kutoa hukumu kuhusu sheria za wafanyikazi na kukataa rufaa yake.

Comments are closed.