UFISADI: MKATABA WA STANBIC NA SERIKALI WAANZA KUCHUNGUZWA

UFISADI: MKATABA WA STANBIC NA SERIKALI WAANZA KUCHUNGUZWA

Like
212
0
Wednesday, 02 December 2015
Local News

SERIKALI imesema imeanza uchunguzi wa ufisadi wa Dola milioni 6 uliohusu mkataba wa mkopo kati ya benki ya Stanbic na serikali.

Jumatatu, mahakama nchini Uingereza iliamuru kulipwa kwa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania baada ya taasisi ya uchunguzi wa makosa makubwa ya ufisadi ya Uingereza kuwasilisha ushahidi kwamba kiasi hicho cha fedha kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za Serikali kwa benki ya Stanbic

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema ni uchunguzi wa benki kuu ya Tanzania katika benki ya Stanbic ndio uliong’amua awali ubadhirifu huo miaka miwili iliyopita.

Comments are closed.