UGANDA: BESIGYE KUACHILIWA HURU

UGANDA: BESIGYE KUACHILIWA HURU

Like
263
0
Friday, 01 April 2016
Global News

MKUU wa kikosi cha polisi nchini Uganda amesema kuwa atawaondoa maafisa wake nje ya nyumba ya kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye mara moja.

Besigye amekuwa akihudumia kifungo cha nyumbani tangu tarehe 20 mwezi Februari,siku ambayo rais Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa taifa hilo.

Hapo jana Alhamisi, Mahakama ya juu nchini Uganda ilitupilia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa rais Museveni.

Comments are closed.