UGANDA NA KENYA ZAIMARISHA USALAMA

UGANDA NA KENYA ZAIMARISHA USALAMA

Like
202
0
Monday, 16 November 2015
Global News

NCHI za Uganda na Kenya zimeimarisha usalama kufuatia mashambulio yaliyojitokeza mjini Paris mwishoni mwa wiki lengo ikiwa ni  kuzuia mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu.

Msemaji wa polisi nchini Uganda amesema polisi na wanajeshi wameimarisha doria kuzuia mashambulio, hasa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab kutoka Somalia.

Nchini Kenya, usalama pia umeimarishwa mipakani na katika miji mikuu, na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka mara wanapoona kitu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka.

Comments are closed.