UGANDA YATENGA BILIONI 20 KUONGEZA MIFUGO

UGANDA YATENGA BILIONI 20 KUONGEZA MIFUGO

Like
628
0
Wednesday, 17 December 2014
Global News

SERIKALI ya uganda imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza mifugo kwenye eneo la Nile Magharibi katika mwaka wa fedha wa 2014 na 2015.

Kwa mujibu wa Kamishna Ofisi ya waziri mkuu anaesimamia mipango ya mifugo Kaskazini mwa Uganda Gonzaga Mayanja, amesema asilimia 97% za fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa mifugo na nyingine kwa gharama za uendeshaji .

Mayanja amebainisha kuwa watoa huduma hizo tayari wamekwisha kusaini mikataba na ifikapo Januari mwakani ugawaji wa mifugo katika Wilaya zilizo wasilisha orodha zao utaanza na kwamba mpango huo una lengo la kuinua uchumi wa nchi na kuwatoa watu katika umaskini.

 

Comments are closed.