UGIRIKI YAJITOA MHANGA KULIKABILI DENI LAKE

UGIRIKI YAJITOA MHANGA KULIKABILI DENI LAKE

Like
222
0
Tuesday, 17 February 2015
Global News

SERIKALI ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.

Mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati serikali ya Ugiriki ilipo tupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Serikali ya Ugiriki inataka kumaliza masharti iliyowekewa katika deni lake la euro bilioni mia mbili na arobaini.

 

Comments are closed.