UHONDO: MSHINDI WA NENO LA KHANGA AKABIDHIWA MILIONI MOJA

UHONDO: MSHINDI WA NENO LA KHANGA AKABIDHIWA MILIONI MOJA

Like
594
0
Friday, 23 October 2015
Local News

Mshindi wa shindano la kubuni neno la Khanga kupitia Uhondo Sekela Richard amekabidhiwa rasmi kitita cha Shilingi milioni moja ya kitanzania.

Shindano hili liliwataka wanawake kushiriki kubuni neno la Khanga kwa kutumia neno Uhondo ambapo njia yake ya ushiriki ilijumuisha makusanyo ya maneno hayo kwa njia ya SMS hadi mshindi kupatikana.

Neon lililotangazwa kuibuka na kura nyingi ni MAMA ANA UHONDO WAKE MTUNZE UPATE MEMA YAKE.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Sekela amesema utunzi wake ulizingatia kushirikisha wanawake zaidi kwenye neon husika.

Mama mzazi wa binti huyu mwenye 18 pia alipata nafasi ya kuzungumza ambapo alieleza furaha yake na kueleza malengo ya kufungua akaunti ya kutunza fedha za mtoto wake ambae ni mwanafunzi

Uhondo inayoongozwa na Dina Marious bado inakupa nafasi mwanamke kuuza khanga iliyobuniwa na kupata asilimia 30% ya kila Khanga unayouza njia ni rahisi chakufanya endelea kusikiliza Uhondo

DU7C4114

 

kushoto ni Meneja wa kitengo cha mawasiliano na mahusiano E-fm Dennis Ssebo akizungumza jambo

DU7C4104

 

picha ni Sekela Richard akizungumza na waandishi wa habari

DU7C4085

Dina Marious mtangazaji wa kipindi cha Uhondo akikabidhi fedha hizo

DU7C4064

 

Dina Marious mtangazaji wa kipindi cha Uhondo akizungumza na waandishi wa habari

DU7C4045

DU7C4037

DU7C4040

DU7C4034

Comments are closed.