UINGEREZA YAWATEMA WANAJESHI 300 WA LIBYA

UINGEREZA YAWATEMA WANAJESHI 300 WA LIBYA

Like
442
0
Thursday, 06 November 2014
Global News

WANAJESHI kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi.

Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi.

Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.

wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.

 

Comments are closed.