UKAGUZI WA MAGARI WAANZA RASMI DAR

UKAGUZI WA MAGARI WAANZA RASMI DAR

Like
407
0
Wednesday, 05 November 2014
Local News

 

JESHI la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam leo limeanza rasmi zoezi la ukaguzi wa magari ikiwa ni pamoja na kufanya makabidhiano ya Stika kutoka kampuni ya Vodacom na Puma ili kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani MOHAMED MPINGA amesema kuwa Stika hizo ambazo ni za magari makubwa, madogo na pikipiki zitasaidia kupunguza ajali baada ya vyombo hivyo kukaguliwa kabla ya kuingia barabarani.

Aidha Kamanda Mpinga amesema kuwa stika hizo ambazo zimeandikwa bei na kupewa namba, huku akiwataka wananchi kutonunua Stika barabara pasipo kukaguliwa ikiwa ni pamoja na kutotoa fedha zaidi ya bei iliyoandikwa katika stika hizo.

Comments are closed.