UKRAINE: HATUA MUHIMU ZA KUSITISHA MAPIGANO ZAFIKIWA

UKRAINE: HATUA MUHIMU ZA KUSITISHA MAPIGANO ZAFIKIWA

Like
194
0
Tuesday, 17 February 2015
Global News

VIONGOZI wa Ujerumani, Urusi na Ukraine wamekubaliana hatua muhimu zitakazowezesha kikosi cha kimataifa cha waangalizi , kuangalia utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine.

Kansela wa Ujerumani ANGELA MERKEL , Rais VLADIMIR PUTIN na mwenzake wa Ukraine , PETRO POROSHENKO , wamezungumza kwa njia ya simu na kujadili njia za kuwaruhusu waangalizi kutoka Shirika la Usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE kuingia katika mji muhimu wa masuala ya usafiri wa treni wa Debaltseve.

Katika eneo la   Mashariki mwa Ukraine mapigano kuzunguka mji muhimu wa Debaltseve yanatishia makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yameanza mwishoni mwa juma.

Comments are closed.