UMOJA WA ULAYA UMESEMA MAHAKAMA NCHINI MISRI IMEKIUKA MAJUKUMU YAKE YA KIMATAIFA

UMOJA WA ULAYA UMESEMA MAHAKAMA NCHINI MISRI IMEKIUKA MAJUKUMU YAKE YA KIMATAIFA

Like
256
0
Tuesday, 03 February 2015
Global News

UMOJA wa  Ulaya  umesema  leo  kuwa mahakama  nchini  Misri imekiuka  majukumu  yake ya   kimataifa  kuhusu  haki  za  binadamu kwa  kuwahukumu  watu 183 adhabu  ya  kifo  jana  kwa  kuwauwa polisi 13.

Idara  ya  mambo  ya  kigeni  ya  Umoja  wa  Ulaya  imesema  katika taarifa yake kuwa  uamuzi  uliotolewa  na  mahakama  ya  Misri kuwahukumu  washitakiwa   183 adhabu  ya  kifo  kufuatia  kesi  ya jumla ni  ukiukaji  wa  majukumu  ya  Misri  ya  haki  za  binadamu.

Hukumu  iliyotolewa  jana , ambayo  inaweza  kukatiwa  rufaa , imekuja  baada  ya  hukumu  za  awali  kupelekwa  kwa  mufti, ambaye  ni afisa  wa  serikali  ya  Misri  anayetafsiri  sheria  za Kiislamu, kwa  ajili  ya  kuidhinishwa.

 

Comments are closed.