Umoja wa Mataifa umeahirisha mazungumzo ya Amani baina ya pande zinazolumbana nchini Libya ambayo yamepangwa kufanyika leo, bila kutangaza tarehe mpya.
Mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika Desemba 9 lakini yamekuwa yakicheleweshwa mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa mapigano kati ya Serikali dhaifu inayotambulika Kimataifa na wapiganaji wanaoungwa mkono na makundi ya Kiislamu.
Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa SAMIR GHATTAS amesema kuwa juhudi zinaendelea kufanyika ili kuyaanda mazungumzo hayo.