UN YATAFAKARI KUTUMA VIKOSI BURUNDI

UN YATAFAKARI KUTUMA VIKOSI BURUNDI

Like
194
0
Thursday, 12 November 2015
Global News

UMOJA wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda Amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi kuendelea.

Watu zaidi ya 200 tayari wameuawa huku maelfu ya wengine wakihama makazi yao tangu Aprili, mara baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Muungano wa Afrika tayari umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa tayari kutumwa Burundi iwapo hali ya Amani itakuwa mbaya zaidi.

Comments are closed.