URUSI YAPOTEZA DOLA BILIONI 40 KUFUATIA VIKWAZO VYA MATAIFA YA MAGHARIBI

URUSI YAPOTEZA DOLA BILIONI 40 KUFUATIA VIKWAZO VYA MATAIFA YA MAGHARIBI

Like
370
0
Tuesday, 25 November 2014
Global News

WAZIRI wa Fedha wa Urusi, ANTON SILUANOV, amesema Urusi imepoteza Dola Bilioni 40 kwa mwaka kutokana na vikwazo ilivyowekewa na nchi za Magharibi kwa madai ya kuhusika katika mzozo wa Ukraine.

Hata hivyo, Rais VLADIMIR PUTIN amesema hasara hiyo sio madhara makubwa kwa Uchumi wa taifa lake.

SILUANOV ambaye alikuwa akitoa hotuba katika Kongamano la Kiuchumi mjini Moscow amebainisha kuwa wamepata hasara ya Mabilioni ya fedha kutokana na vikwazo vinavyohusishwa na siasa za Urusi kuelekea eneo hilo na kuongeza kuwa kuporomoka kwa bei ya mafuta kunasababisha uchumi wa Urusi kupata hasara ya kati ya dola bilioni 90 na 100 kwa mwaka.

 

Comments are closed.