Urusi yateka meli za kivita za Ukraine

Urusi yateka meli za kivita za Ukraine

Like
655
0
Monday, 26 November 2018
Slider

Urusi imezishambulia na kuziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea katika kisa ambacho kimezidisha uhasama baina ya mataifa hayo mawili.

Jeshi la wanamaji la Ukraine linaituhumu Urusi kwa kushambulia na kuharibu moja ya meli zake za kivita

Meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi.

Wahudumu kadha wa meli za Ukraine wamejeruhiwa.

Kila taifa linamlaumu mwenzake kwa kusababisha kisa hicho.

Leo Jumatatu, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.

Mzozo wa sasa ulianza pale Urusi ilipoituhumu Ukraine kwa kuingiza meli katika maeneo yake ya bahari kinyume cha sheria.

Urusi kisha iliweka meli kubwa ya kusafirisha mizigo na kuziba daraja la kuingia kwenye mlango wa bahari wa Kerch, njia pekee ya kuingia kwenye Bahari ya Azov na ambayo hutumiwa na mataifa yote mawili.

Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama na Ulinzi la Ukraine, Rais Petro Poroshenko alieleza vitendo vya Urusi kuwa “uchokozi usio na sababu na za kiwendawazimu.”

Urusi imeomba kuandaliwe mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mkutano ambao balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema umepangiwa kufanyika saa tano asubuhi saa za New York (16:00 GMT) leo Jumatatu.

Uhasama umekuwa ukiongezeka katika Bahari Nyeusi na Bahari ya Azov katika rasi ya Crimea, eneo lililotekwa na Urusi mwaka 2014 kutoka kwa Ukraine.

Mzozo wa sasa umetokeaje?

Asubuhi, meli za kivita za Berdyansk na Nikopol, pamoja na meli ya kuzisindikiza Yana Kapa, zilijaribu kusafiri mji wa bandarini kwenye Bahari Nyeusi wa Odessa kuelekea Mariupol katika Bahari ya Azov.

Ukraine inasema Urusi ilijaribu kuzizuia meli hizo zisiendelee na safari yake, ambapo meli moja iliigonga meli ya Yana Kapa.

Meli hizo ziliendelea na safari kuelekea mlango wa bahari wa Kerch, lakini zikapata njia imezibwa na meli moja kubwa.

Urusi wakati huo ilikuwa imetuma ndege mbili za kivita na helikopta mbili ambazo zilikuwa zikipaa angani katika eneo hilo na kufuatilia mwenendo wa meli hizo.

Urusi inaituhumu Ukraine kwa kuingia kinyume cha sheria katika maeneo yake ya bahari na usafiri eneo hilo umesitishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu za kiusalama.

Jeshi la wanamaji la Ukrane lilisema meli hizo zilikuwa zimeshambuliwa na kuharibiwa zilipokuwa zinajaribu kuondoka eneo hilo.

Imesema wahudumu wake sita wamejeruhiwa.

Jeshi la wanamaji la Urusi lilizizuia meli hizo za Ukraine baada ya kuzituhumu kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye maeneo ya bahari ya Urusi

Idara ya Usalama ya Urusi ifahamikayo kama FSM, ambayo inatekeleza mengi ya majukumu yaliyotekelezwa na KGB, ilithibitisha baadaye kwamba moja ya boti zake za kushika doria baharini ilitumia nguvu kuchukua udhibiti wa meli tatu za Ukraine.

Lakini walisema ni mabaharia watatu pekee waliojeruhiwa.

Ukraine imesema ilikuwa imeifahamisha Urusi kuhusu mpango wake wa kupitishia meli hizo zake eneo hilo kuelekea Mariupol.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *