UTURUKI YAOMBOLEZA VIFO VYA WATU 95

UTURUKI YAOMBOLEZA VIFO VYA WATU 95

Like
252
0
Monday, 12 October 2015
Global News

MAELFU ya Watu wamekusanyika mjini Ankara nchini Uturuki kuomboleza vifo vya takriban watu 95 waliouawa kwa milipuko miwili ya mabomu.

Watu wanaounga mkono Chama cha Kikurdi ambao walikuwepo kwenye mkutano katika eneo ambalo mabomu yalilipuka wanaamini kuwa idadi ya kweli ya waliopoteza maisha ni Watu 128.

Vyanzo vya ulinzi vinasema kuwa vinalishuku kundi la wanamgambo wa IS kuhusika kwenye shambulio hilo huku Serikali ikikanusha vikali madai kuwa imehusika katika mashambulizi hayo.

Comments are closed.