UVUVI HARAMU KWA NJIA YA SUMU HATARI KWA MAISHA YA WATU UKEREWE

UVUVI HARAMU KWA NJIA YA SUMU HATARI KWA MAISHA YA WATU UKEREWE

Like
256
0
Wednesday, 26 August 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa uvuvi haramu kwa njia ya sumu wilayani Ukerewe unahatarisha maisha ya watu kwa kuugua ugonjwa wa ini na figo huku wengine wakipoteza maisha kwa ugonjwa huo.

 

Wakiongea na Efm baadhi ya wakazi  wa ukerewe   walioathirika na ulaji wa  samaki waliovuliwa kwa sumu wamesema uvuvi haramu ndio chanzo cha wao kuugua ugonjwa wa ini na figo na kufanya familia zao kuishi kwa taabu.

 

Kwa upande wake daktari kutoka katika hospitari ya rufaa Bugando jijini mwanza  Mathayo James amekiri kuwepo kwa  tatizo hilo.

Comments are closed.