Venezuela imesema imemuita balozi wake mjini Washington MAXIMILIEN SANCHEZ arejee nyumbani baada ya vikwazo vya Marekani dhidi ya maafisa wake.
Rais wa Venezuela NICOLAS MADURO ameikosoa vikali Marekani kwa kuwawekea vikwazo maafisa wa Venezuela wanaoshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu, akisema ataliomba bunge limpe mamlaka zaidi kupambana na kitisho cha ubeberu.