VIDEO YA BOKO HARAM YAONESHA WASICHANA NA CHIBOK

VIDEO YA BOKO HARAM YAONESHA WASICHANA NA CHIBOK

Like
282
0
Thursday, 14 April 2016
Global News

KANDA ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram imewaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wakiwa hai.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba ni kipindi cha miaka miwili sasa tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok nchini humo.

Hata hivyo ni wasichana 15 tu, wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya sikukuu ya Krismasi mwaka jana.

Comments are closed.