Vijana 12 waliokwama pangoni kwa siku 9 Thailand wapatikana hai

Vijana 12 waliokwama pangoni kwa siku 9 Thailand wapatikana hai

Like
447
0
Tuesday, 03 July 2018
Global News

Video fupi imetolewa ikiwaonesha wajumbe wajumbe wa kikosi cha timu ya soka ya Thailand waliokutwa wakiwa hai ndani ya pango lililotandaa na pia lililo fura maji .

Kugunduliwa na kuokolewa kwa wavulana kumi na wawili na kocha wao mmoja wakiwa hai baada ya siku tisa za kunaswa katika pango upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Thailand kumesababisha kuwa gumzo katika vyombo mbali mbali vya habari ulimwenguni. Sauti ya kwanza kuisikia baada ya siku tisa ni ya bwana Briton John Volanthen.

Bwana Volanthen na Richard Stanton waliitwa na mamlaka za Thailand pamoja na mtaalamu wa mapangoni kutoka nchini Uingereza, Robert Harper.

Baraza la uokozi mapangoni kutoka nchini Uingereza wamearifu kuwa watatu hao waliwasili nchini Thailand siku tatu baada ya timu hiyo ya mpira kuelekea katika mapango ya Tham Luang katika mji wa Chiang Rai mahali ambako walikwenda kwenye matembezi ya kujifurahisha.

Baraza hili liliarifu kuwa mapango mengi nchini humo yanaratibiwa na wataalamu wa uokozi mapangoni kutoka nchini Uingereza, ambao hutoa uzoefu wao kutokana na kazi walizowahi kuzifanya mahali kwingine ulimwenguni.

Vijana hao wanaonekana wakiwa wamekaa katika kijisehemu cha ardhi huku wakiwa wamezunguukwa na maji, ndani kabisa ya pango mahali ambako walikwama kwa muda wa siku tisa, huku mashati yao yakiwa magotini, wavulana hao walisikika wakiomba chakula na kuondoka katika pango hilo haraka iwezekanavyo na mara juhudi za kuokozi kufanikisha zoezi hilo la uokozi, vijana hao walitoa shukrani zao za dhati.

Zoezi hilo halikuwa rahisi kwa muujibu wa kikosi cha uokozi, kwani maji mara kwa mara yalikuwa yanajaa , huku tope nalo likiongeza ugumu katika zoezi hilo. Kikosi cha majini cha uokozi kutoka Uingereza ndicho kilichokuwa cha kwanza kuwasili, na hatua ya kwanza waliyofanya ni kuwatuliza kisaikolojia vijana hao kwa kuwaeleza kuwa wao ni wa kwanza kuwasili hapo na hivyo msaada zaidi unafuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *